Saido moto wa kuotea mbali, Simba ikishinda kiducuu

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC jioni ya leo imeifunga timu ya KMC ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kuilaza bao 1-0 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha mchezo wa Ligi Kuu bara.

Licha ya ushindi huo Simba bado inaendelea kushika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 ikizidiwa na magoli ya kufunga na Azam ambayo leo imeichapa Kagera Sugar mabao 5-1 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Goli pekee la Simba lilifungwa dakika ya 2 na Said Ntibanzokiza "Saido", mechi nyingine zilizochezwa leo ni Yanga 3 Tabora United 0
Azam 5 Kagera Sugar 1
Mashujaa 3 Mtibwa Sugar 2
Ihefu 0 Dodoma Jiji 1
Singida FG 2 Geita Gold 1
Namungo 2 Prisons 2
Coastal Union 0 JKT Tanzania 0


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA