Winga Simba akoleza usajili wa Abdul Machela Coastal Union
Mchezaji wa zamani wa Simba SC Said Msasu amewaambia Coastal Union kwamba wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Black Bulls Lichinga ya Msumbiji Abdul Machela hawatakosea kwani anamjua dogo huyo ni moto wa kuotea mbali.
Msasu ambaye aliwahi kuichezea Simba akitokea timu ya Friends Rangers ya Magomeni Kagera, anamjua vizuri Machela kwani aliwahi kumpeleka African Sports ya Tanga wakati yeye akiinoa
Machela ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Simba SC, Ally Machela, anatajwa kujiunga na Coastal Union ya Tanga ambayo tayari ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho msimu ujao baada ya kumaliza nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu bara.
Mbali na Coastal Union kumuwania Machela, Ihefu SC nayo inatajwa kumchukua kiungo huyo lakini pia timu yake ya Black Bulls imepanga kumuongeza mkataba ili kumbakisha
Msasu aliandika yafuatayo: "Mmoja wa viungo bora kwa sasa namfuatilia sana tokea aende Msumbiji niliewahi kumpitisha kusajiliwa African Sports