Al Ahly na ubingwa wa 12 Ligi ya mabingwa Afrika
Klabu ya Al Ahly ya Misri imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya 12 kufuatia ushindi wa jumla wa 1-0 dhidi ya Esperance ya Tunisia.
Bao pekee la kujifunga la Roger Aholou dakika ya 4 limetosha kuwapa ubingwa Ahly.
Mchezo wa fainali ya kwanza iliyopigwa Tunisia ulimalizika kwa sare tasa kabla ya Al Ahly kutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kushinda 1-0 nyumbani.
Al Ahly wanatwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita