Joseph Guede hatihati kubaki Yanga
Mshambuliaji wa Yanga SC Joseph Guede amethibitisha kuwa mkataba wake na Yanga unamalizika Mwezi June mwaka huu lakini Hatma ya yeye kusalia kwenye Kikosi cha Yanga anamuachia Rais wa Yanga Engineer Hersi Said.
Guede ambae alijiunga na Yanga wakati wa Dirisha dogo la usajili 2023/2024 alisaini kandarasi ya miezi sita ndani ya viunga vya Jangwani.
Guede amethibitisha hayo wakati akifanya mahojiano na Crown Media wakati wa sherehe za Ubingwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.