Diarra ashinda tuzo Afrika
Golikipa wa Klabu ya Yanga, Djigui Diarra ameshinda tuzo ya mchezaji bora Afrika msimu 2023/2024, tuzo hizi maalumu hutolewa nchini Mali kwa wachezaji wao waliofanya vizuri kwa msimu husika (Mali Football Awards).
Diarra ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Sadio Kanoute kiungo mkabaji wa Simba, Fily Traore mshambuliaji wa TP Mazembe, Aliou Dieng kiungo mkabaji wa Al Ahly na Abdoulaye Kanou mshambuliaji wa USM Alger.