Bwalya na Wydad kimeeleweka
Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Nkana Rangers ya Zambia, Al Ahly ya Misri na Wydad Casablanca ya Morocco, Walter Bwalya ameamua kuondoa kesi yake FIFA na kukubaliana kuvunja mkataba.
Bwalya aliishitaki Wydad Casablanca, FIFA, lakini amekaa chini na kuongea na viongozi wa klabu hiyo hatimaye wamekubaliana kumalizana hivyo akaamua kuondoa kesi hiyo na klabu ikaamua kuvunja mkataba wake
Kwasasa Bwalya Ni mchezaji huru na anaweza kujiunga na klabu yoyote anayoitaka