Yanga kumng' oa Chama kwa milioni 200
Klabu ya Yanga imempa ofa ya milioni 200 ya ada ya usajili na mshahara wa milioni 20 kwa mwezi kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia na klabu ya Simba SC, Clatous Chama ili asaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mmoja zaidi.
Chama mwenye umri wa miaka 32 yupo tayari kusaini mkataba Yanga mara baada ya mkataba wake na Simba kuisha.