John Bocco atundika daruga
John Bocco ametangaza kustaafu soka baada ya kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa zaidi ya Misimu 16.
Bocco amefanikiwa kufunga magoli zaidi 100+ kwenye Ligi Kuu na kuwa Mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye historia ya Ligi Kuu.
Mshambuliaji huyo aliyeibukia Cosmopolitan iliyokuwa inashiriki Ligi daraja la pili, alijiunga na Azam FC na alifanikiwa kuipandisha Ligi Kuu na pia kuipa ubingwa wa Ligi Kuu bara.
Msimu wa 2017/2018 alijiunga na Simba na kuwapa mafanikio kadhaa na ameamua kustaafu na kujikita kwenye ukocha na sasa anafundisha timu ya vijana ya Simba B