SIRI ZA AZIZ KI KUIBA UCHAWI WA PACOME ZAVUJA
Na Mwandishi Wetu
Kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz Ki raia wa Burkina Faso ni kama amechukua uchawi wa kiungo mwenzake Pacome Zouzoua raia wa Ivory Coast.
Pacome kabla hajaumia alikuwa mchezaji kipenzi cha Wanayanga na alikuwa akicheza kwa umahiri wa hali ya juu, Aziz Ki na umahiri wake wa kupiga mashuti makali bado alikuwa hamfikii Pacome.
Pacome ana mtindo wake wa kupaka rangi nyeupe nywele zake na zilimpatia umaarufu mkubwa, kuna wakati nywele hizo za rangi nyeupe zilionekana kama uchawi wake ndani ya uwanja.
Aziz Ki alianza kupaka rangi nyeupe wakati Yanga ilipompa Pacome mechi yake moja iliyoitwa Pacome Day ambapo Yanga ilicheza na CR Belouizdad ambapo Yanga ilishinda mabao 4-0.
Kuanzia hapo Aziz Ki hakuacha kupaka rangi na akaendelea hivyo mpaka sasa, nyota ya Aziz Ki ikawa juu huku ya Pacome ikazima, kwasasa Aziz Ki anapendwa zaidi kwenye kikosi cha Yanga wakati Pacome anaonekana wa kawaida