Tuzo za Ligi Kuu msimu huu kutolewa msimu ujao
Taarifa ya TFF iliyotolewa leo inasema hivi:- "Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sasa zitakuwa zikifanyika wakati wa michezo ya
Ngao ya Jamil.
Lengo la mabadiliko ya Hafla hizo za kuwatuza wachezaji bora wa msimu ni kufanya maboresho ya kulifanya tukio kuwa bora zaidi kukidhi malengo na mahitaji yake.
Kwa mabadiliko hayo hafla ya Tuzo za TFF kwa msimu wa 2023/2024 itafanyika wakati wa michezo ya
Ngao ya Jamii kufungua msimu wa 2024/2025.
Tuzo za TFF ni tukio la kuzawadia wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano yanayoandaliwa na TFF/Bodi ya Ligi (TPLB) na matukio mengine rasmi yenye kuambatana na mpira wa miguu hapa chini.
@hajismanara akaandika haya kwenye Insta yake:- "Viongozi wangu Wapendwa sana naogopa hata kuwashauri nisije kuonekane Bindeli, lakini haijawahi kutokea duniani kote tuzo za msimu huu zitolewe msimu
ujao.
Ngao ya Jamii ni mwanzo wa msim na mmeamua tuzo za
msimu huu tulionao mzipeleke next season, mmetumia kigezo gani hasa Shirikisho?
Imagine Wachezaji wengine labda watahama team na tuzo binafsi zinahusiana direct na team yake coz wenzie kikosini na bench lake la ufundi wana mchango wao kwake, itakuwaje hapo ?
Lakini pia kuzihamisha tuzo za msimu huu kuzipeleka msimu ujao kutatengeneza maswali mengi iwapo
Ahhh ikiwapendeza Wakubwa wa Mpira wapeni chao wanaostahili kupewa hizo tuzo kabla hawajaanza likizo ili