Simba na Azam zamgombea mshambuliaji wa San Pedro
Simba SC na Azam SC zote zimeulizia upatikanaji wa huduma ya mshambuliaji wa kati raia wa Ivory Coast ambaye kwa sasa anakipiga SAN PEDRO FC, Bedi Guy Stephanie (28).
Mshambuliaji huyo mzoefu amekuwa katika kiwango kizuri tangu asajiliwe San Pedro kwani msimu huu ameshinda kiatu cha mfungaji bora akiwa na mabao 15.
MCB MICHEZO, HERE WE GO 🤝👊🫵🛜💻