FAR Rabat yamtengea Inonga milioni 62 kwa mwezi
Taarifa kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika zinadai kuwa FAR Rabat ya nchini Morocco imemuandalia mshahara wa zaidi Tsh million 62 kwa mwezi mlinzi Henock Inonga Baka endapo atakubali kujiunga na miamba hiyo ya nchini Afrika Kaskazini.
Tetesi zimekuwa zikamhusisha nyota huyo kujiunga na AS FAR Rabat na inaelezwa alishafikia makubaliano na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Morocco 'Botola Pro' toka Kipindi Cha michuano ya AFCON.