Mo Dewji kuinunua Express ya Uganda
Mfadhili Wa Simba sc na Tajiri namba 17 barani Afrika Mohammed Dewji Yuko mbioni kununua Hisa asilimia 51% katika Klabu ya Express FC ya nchini Uganda.
Baada ya kuwekeza katika Klabu za Tanzania sasa ni rasmi Mohamed amedhamiria kuwekeza Uganda.
Express FC msimu huu imeshika nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi iyo ikiwa na jumla ya Alama 32 Ikiwa imefunga Magoli 36 na kuruhusu Magoli 38.