Ligi inachezwa msimu huu, zawadi msimu ujao

Na Prince Hoza

INASHANGAZA sana zawadi za washindi wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu wa 2023/2024 kupewa msimu ujao wa 2024/2025.

Bodi ya Ligi pamoja Shirikisho la soka nchini, TFF limetangaza jana kwamba litatoa tuzo za washindi wa msimu huu wa Ligi Kuu bara.

Bodi ya Ligi wamepanga kutoa tuzo hizo siku ya fainali ya Ngao ya Jamii msimu ujao, ikumbukwe Ngao ya Jamii ni ya kuashiria kuanza kwa msimu mpya.

Malalamiko yamekuwa mengi juu ya maamuzi hayo ya kuwapa tuzo washindi wa msimu huu siku ya Ngao ya Jamii, wadau wanashangazwa sana uamuzi huo wakiamini TFF na Bodi ya Ligi haiwatendei haki wanaostahili kutunukiwa.

Stephanie Aziz Ki mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara aliyepachika mabao 21 alistahili kupewa tuzo yake baada ya kumalizika ligi hiyo.

Kumchelewesha sio sawa, ni uonevu juu yake, Aziz Ki ni raia wa Burkina Faso kwa vyovyote anarejea kwao hasa kwa sababu msimu umemalizika na mkataba wake na Yanga umeisha.

Haijajulikana kama Aziz Ki ataendekea kuichezea Yanga, kwani zipo tetesi kwamba anahitajika na timu zaidi ya moja, kama ataondoka itakuwa ngumu kumuona anakuja kufuata tuzo yake hivyo ni sawa na kutomtendea haki.

Aziz Ki alifanya kazi kubwa kushindania kiatu kwani alikutana na upinzani mkali kutoka kwa Feisal Salum "Feitoto" ambaye ikiwa imebaki mechi moja ligi kumalizika wote wawili walifungana kwa magoli 18.

Mwishoni mwa ligi Aziz Ki aliibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao matatu na kufikisha magoli 21, lakini pia mlinda mlango Let Matampi raia wa DR Congo ambaye anaweza kutajwa kama golikipa bora msimu huu alistahili kupewa tuzo yake baada ya ligi kumalizika

Kumpa tuzo yake msimu ujao si haki, ifahamike wazi kwamba msimu unapomalizika timu zinafanya maboresho ya vikosi vyao hivyo kuna klabu zitalazimika kuwasajili wachezaji wengine.

Hivyo wapo nyota wa timu nyingine watahamia kwingine hivyo tuzo yake itabidi ichukuliwe na mtu wa upande mwingine, ni ngumu kwa mchezaji kama Matampi achukue tuzo akiwa anaichezea Simba au Yanga ilihali aliipatia akiwa Coastal Union.

Sawa na Aziz Ki achukue tuzo akiwa Simba wakati aliipata akiwa Yanga, kuna namna Bodi ya Ligi wanatakiwa kuwatendea haki wadau waliostahili kupewa tuzo zao wakati muafaka, kuvhelewesha tuzo zao ni uonevu kama uonevu mwingine.

Sijajua ni kwanini Bodi ya Ligi imefanya hivyo, ni ukosefu wa zawadi za washindi au makusudi kwa sababu kuna watu flani walitakiwa kupata lakini wakazikosa.

Kama ni makusudi basi wanatakiwa wasifanye hivyo kwani mpira hauendeshwi kwa matakwa ya mtu bali vitungu vya sheria na kanuni, mwisho nawaomba Bodi ya Ligi na TFF muendelee kujifunza kwa waliopiga hatua.

ALAMSIKI


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA