Siri zavuja, Kessy aibwaga Simba
Na Mwandishi Wetu Dalili za beki Hassan Ramadhan Kessy kukipiga Yanga bila vikwazo huenda ikafanikiwa baada ya kamati iliyoketi hivi karibuni iliyoongozwa na wakili Richard Sinamtwa kuitaka Klabu ya Simba kuwasilisha vielelezo kama imewahi kumlipa beki huyo mshahara wake wa miezi mitatu kupitia akaunti yake ya benki. Endapo Simba itashindwa kuwasilisha vielelezo hivyo basi beki huyo atakuwa ameibwaga Klabu yake hiyo ya zamani kwani kesi hiyo itatupiliwa mbali. Mwanasheria wa Yanga, Alex Mgongolwa ndiye aliyeiomba kamati hiyo kuhoji kama ni kweli Simba walikuwa na uhalali wa kummiliki mchezaji huyo, hata hivyo kesi hiyo bado inapigwa danadana