Siri zavuja, Kessy aibwaga Simba

Na Mwandishi Wetu

Dalili za beki Hassan Ramadhan Kessy kukipiga Yanga bila vikwazo huenda ikafanikiwa baada ya kamati iliyoketi hivi karibuni iliyoongozwa na wakili Richard Sinamtwa kuitaka Klabu ya Simba kuwasilisha vielelezo kama imewahi kumlipa beki huyo mshahara wake wa miezi mitatu kupitia akaunti yake ya benki.

Endapo Simba itashindwa kuwasilisha vielelezo hivyo basi beki huyo atakuwa ameibwaga Klabu yake hiyo ya zamani kwani kesi hiyo itatupiliwa mbali.

Mwanasheria wa Yanga, Alex Mgongolwa ndiye aliyeiomba kamati hiyo kuhoji kama ni kweli Simba walikuwa na uhalali wa kummiliki mchezaji huyo, hata hivyo kesi hiyo bado inapigwa danadana

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI