Smart Sport yaikalia kooni TFF, sasa yataka kuipoka basi kufidia deni lake
Na Prince Hoza, Dar es Salaam
Kampuni ya kuuza na kusambaza vya michezo ya Smart Sport imetishia kwenda mahakamani ili ikamate mali za Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) ambao eanawadai mamilioni ya shilingi.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa kampuni hiyo George Wakuganda amesema watalifikisha mahakamani Shirikisho hilo ili waweze kuwapoka basi lao kama hawatalipwa fedha zao.
Smart Sport ndiyo iliyokuwa ikisambaxa vifaa vya michezo kwenye Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) ambapo timu zote za taifa zilikuwa zikitumia vifaa hivyo