TP Mazembe yabeba ndoo ya Shirikisho Afrika

Na Prince Hoza, Lubumbashi

TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidenokrasia ya watu wa Kongo, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 na kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika.

Fainali ya leo ilikuwa ya pili kwani miamba hiyo iliwahi kukutana katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika uwanja wa Stade Mustapha Tchaker Algeria.

TP Mazembe hadi wanakwenda mapumziko walikuwa mbele kwa mabao mawili yaliyofungwa na Bokadi dakika ya 7 na Kalaba dakika ya 43.

Mabao mengine yalifungwa kipindi cha pili yakifungwa tena na Kalaba dakika 62 na Bolingi dakika ya 77, lile la Bejaia lilifungwa na Khadir dakika ya 75

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA