Simba kweli baiskeli la miti, yakalishwa 2-1 Sokoine

Na Exipedito Mataruma, Mbeya

Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC leo jioni imeendelea kudhihirisha kuwa ni baiskeli ya miti baada ya kulazwa 2-1 na Tanzania Prisons  katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mchezo wa Ligi kuu bara, mabao mawili ya Koplo Victor Hangaya yalitosha kabisa kuisinamisha Simba kuzidi kuikimbia Yanga kileleni, kwa maana hiyo Yanga inahitaji kushinda kesho dhidi ya Ruvu Shooting ili kuisogelea Simba, hii ni mechi ya pili Simba inalala baada ya Jumapili kufungwa na African Lyon 1-0 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Simba walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa dakika ya 43 kipindi cha kwanza likifungwa na Jamal Mnyate, kipigo hicho ni cha pili na kufanya iendelee kusimama na pointi zake 35 kwa mechi 15.

Kesho Yanga watakutana na Ruvu Shooting uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, lakini hata kama watashinda hawataweza kuishusha Simba, Azam FC nayo imeamka kule mjini Shinyanga katika uwanja wa Mwadui baada ya kuichabanga Mwadui mabao 4-1 na kushikilia nafasi ya pili kwa pointi 25 mechi 15



Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA