Kivumbi Ligi Kuu Bara leo, Yanga kukinukisha na Prisons, Simba na Lyon

Na Saida Salum

Kinyang' anyiro cha Ligi Kuu Tanzania bara kinaendelea leo kwa mechi nane kupigwa katika viwanja tofauti hapa nchini.

Kule Manungu mjini Morogoro, wenyeji Mtibwa Sugar watawaalika Mbeya City kiboko wa Yanga, wakati katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, African Lyon watawakaribisha Wekundu wa Msimbazi, Simba SC.

Mwadui wakitumia uwanja wao wa Mwadui kule Shinyanga watawaalika Majimaji ya Songea, Mbao FC ya Mwanza itautumia uwanja wa CCM Kirumba kuwakaribisha Azam FC ya Chamazi Dar es Salaam, na Ndanda ya Mtwara itawakaribisha Stand United 'Chama la wana' kule Nangwanda Sijaona.

Kipute kitakuwa jijini Mbeya masarange wa Prisons wakiwakaribisha mabingwa watetezi ambao wanasuasua msimu huu Yanga SC ambao leo wameapa kukinukisha kwani Jumatano iliyopita walifungwa mabao 2-1 na Mbeya City.

Kagera Sugar wakitumia uwanja wao wa Nyasi bandia wa Kaitaba watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting ya Masau Bwire na JKT Ruvu watacheza uwanja wao wa Mabatini kuwakaribisha Toto Africans

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA