Simba sasa hii sifa!
Na Prince Hoza, Shinyanga
Simba SC wameendelea kulifukuzia kwa mwendokasi taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ngumu msimu huu Stand United ya Shinyanga.
Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 35 baada ya kucheza mechi 13, wakati Stand inabaki na pointi zake 22 za mechi 14.
Bao lililoipa ushindi Simba lilifungwa na winga machachari wa Wekundu hao wa Msimbazi Shiza Ramadhan Kichuya kwa mkwaju wa oenalti katika dakika ya 33 baada ya Mrundi Laudit Mavugo kuangushwa na beki Adeyuni Ahmed kwenye boksi