Tshabalala aongeza miaka miwili Simba
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam
Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba SC, leo wamemuongezea mkataba wa miaka miwili beki wao wa kushoto Mohamed Hussein 'Tshabala' (21) na kumfanya asalie mpaka mwaka 2018.
Tshabalala ameongeza mkataba huo wa miaka miwili hii leo katika ofisi za Rais wa Klabu hiyo Evans Elieza Aveva, kwa maana hiyo zile tetezi zilizokuwa zikivumishwa kwamba beki huyo ataelekea mitaa ya Jangwani sasa zimezimwa.
Simba inaendelea kumalizana na nyota wake ambao mikataba yao inaelekea ukingoni, Nahodha wa timu hiyo Jonas Mkude naye anaweza kumalizana na uongozi wa Simba kama ilivyokuwa kwa Tshabalala