Kiungo mzuiaji wa Zesco United laja kumrithi Domayo Yanga
Na Prince Hoza, Dar es Salaam
Hatimaye mabingwa wa soka nchini Yanga SC wako mbioni kumleta kiungo wa Zesco ya Zambia ili kumrithi kiungo Frank Domayo 'Chumvi' ambaye pengo lake mpaka sasa bado halijazibwa.
KIUNGO mkabaji na mchezaji wa kutegemewa wa Zesco United, Meshack Chaila yupo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wake kutua Young African SC! Chaila raia wa Zambia anasifika kwa kucheza soka kazi, mzuri katika ulinzi na kuharibu mipango ya timu pinzani.
Yanga SC imepigana vikumbo na vilabu vya Misri kuwania saini ya nyota huyo, Chaila amewekewa mezani mkataba wa miaka 2 na huenda Yanga wakakamilisha usajili wake mapema wiki hii.