Okwi anarejea Msimbazi, Yanga matumbo joto

Na Nasri Alfan, Dar es Salaam

Kiungo mshambuliaji Emmanuel Anord Okwi raia wa Uganda, anatarajia kutua Msimbazi kujiunga na vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba SC kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Okwi tayari alishajiunga na Sobderjsky ya Denmark inayoshiriki Ligi Kuu lakini wamekubaliana na Simba kwamba watauvunja mkatana wao, Klabu hiyo imewataka Simba kuwarudishia fedha zao Dola laki mbili walizomnunulia awali.

Uongozi wa Simba nao umeridhia kulipa fedha hizo na sasa kiungo huyo mshambuliaji atarejea kunako Klabu yake ya zamani, Okwi anakumbukwa vema na mahasimu zao Yanga kwani amewahi kuwafunga mara kadhaa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA