Clinton wa Yanga afariki dunia

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Klabu ya Yanga yenye maskani yake jijini Dar es Salaam, Isaack Shekiondo maarufu kama Clinton amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Taarifa iliyotolewa na familia inasema kwamba msiba upo nyumbani kwake Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam, marehemu alikuwa akiugua kwa muda.

Enzi zake katika miaka ya 2000, Clinton aliyebatizwa jina hilo baada ya kuonekana mwenye misimamo kama aliyokuwa nayo Rais wa wakati huo wa Marekani Bill Clinton, marehemu Clinton alikuwa makamu wa mwenyekiti wa Yanga anayekumbukwa vema kwa kuanzisha mchakato wa kampuni.

Marehemu enzi zake alifanya kazi pamoja na Tarimba Abbas Tarimba na kuifanya Yanga iwe kwenye maendeleo makubwa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA