Ivo Mapunda aanzisha kituo chake cha michezo, lengo kuondoa Panya Road
Na Prince Hoza, Dar es Salaam
Kipa wa zamani wa Yanga, Simba na Taifa Stars, Ivo Philip Mapunda, ameamua kuanzisha kituo chake cha michezo kitakachojumlisha vijana kuanzia umri wa miaka 8- 18.
Akizungumza jana, Mapunda amesema amefikia maamuzi hayo hasa baada ya kuona vijana wengi wakijihusisha na vitendo vya kihuni kama 'Panya Road' na makundi mengineyo.
Kipa huyo aliyewahi pia kuzichezea Tukuyu Stars, Prisons, Moro United, African Lyon, Bandari Mombasa, Gor Mahia, St George na pia Azam FC, kipa huyo amedai bado hajaamua kustaafu soka na amevitaka vilabu vinavyomuhitaji yupo tayari kujiunga nazo