Yanga yakalishwa 2-1 na Mbeya City
Na Ikram Khamees, Mbeya
Mbeya City FC imeutumia vema uwanja wake wa Sokoine mjini Mbeya baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Yanga mabao 2-1.
Ushindi huo wa kwanza kwa Mbeya dhidi ya Yanga tangu wapande Ligi Kuu, unaifanya Mbeya City ifikishe pointi 19 baada ya kucheza mechi 14 wakati Yanga inabaki na pointi zake 27 za mechi 13.
Mabao ya Mbeya City yalifungwa kipindi cha kwanza na Hassan Mwasapili na nahodha Kenny Ally, na goli moja la Yanga nalo lilifungwa kipindi cha kwanza na mshambuliaji wake Mzimbabwe Donald Ngoma, Yanga wanaendelea kukaa nafasi ya pili