Azam FC waanza kujiimarisha,yamsainisha miaka mitatu Mghana
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam FC, imemsainisha mkataba wa miaka mitatu kiungo wa zamani wa Medeama ya Ghana, Enock Atta Agyei.
Kiungo huyo aliyetimiza miaka 18, ameruhusiwa kujiunga na Azam baada ya awali kukataliwa kwa sababu hakuwa na miaka 18 kwani sheria za Ghana haziruhusu mchezaji kucheza nje ya Ghana.
Klabu hiyo inayokamata nafasi ya tatu ikiwa na pwenti 25 ikizidiwa pointi kumi na kinara wa ligi hiyo Simba ambao wana pointi 35, timu hiyo msimu huu imeonekana si tishio kama ilivyokuwa misimu iliyopita