Azam FC awalembi, yabeba Waghana wawili
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
AZAM FC jana imewasajili wachezaji wawili wa kimataifa kutoka nchini Ghana, nshambuliaji Samuel Afful na kiungo Yahaya Mohamed wametia saini kuitumikia Azam katika mzunguko wa pili.
Mabingwa hao wa Afrika mashariki na kati tayari wameshawasaini Waghana watatu wakianza na Enock Atta Agyei ambaye alikuwa akiichezea Medeama.
Azam imeachana na maproo wake watatu ambao ni Kipre Michael Balou, Kipre Herman Tchetche na Paschal Wawa ambao wote ni raia wa Ivory Coast