USHAHIDI WA PICHA: MASHALI KUMBE ALISILIMISHWA NA SHEIKH SHARIFU
Picha/Habari na Salum Fikiri Jr
Bondia Thomas Mashali ambaye jana alizikwa katika makaburi ya Kinondoni kwa dini ya Kikristo dhehebu la Katoliki kumbe siku za hivi karibuni alibadili dini na kuingia Uislamu.
Mbaruku Heri ambaye naye ni bondia na kocha wa mchezo huo, amethibitisha kuwa Thomas Mashali ni muislamu lakini anashangaa kuzikwa kikristo, bondia huyo aliamua kusilimu yeye mwenyewe na Sheikh aliyehusika kumbadili ni Sharifu.
Heri anadai kuwa bondia huyo aliamua aitwe Mohamed Mashali, lakini anasikitika kuona akizikwa kwa dini ya Kikristo aliyoikataa marehemu mwenyewe, Heri anasema iko wapi haki ya Waislamu mbona wapo Waislamu walioamua kuingia Ukristo na wakifa wanazikwa Kikristo, Heri anasema kuna kaubaguzi kidogo hapa nchini