Rage ampiga kijembe Malinzi
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Aliyekuwa mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Alhaj Ismail Aden Rage amempiga kijembe Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi kwambs si mtu wa mpira na ndio maana katika utawala wake tunashuhudia Tanzania ikiporomoka katika viwango vya ubora huku hali ikizidi kuwa mbaya.
Rage amesema viongozi wa sasa wengine walikuwa wanaongoza masumbwi na anashangaa kuwaona wakiliongozs soka. Malinzi ndiye aliyekuwa akiongoza masumbwi, enzi zake akimpromoti bondia Rashid Matumla kupitia kampuni yake ya DJB Promotion.
Kwa sasa Malinzi ameshindwa kuivusha Tanzania kwani timu zake zote za Taifa zimetolewa kwenye mashindano iliyoshiriki, pia tumeshuhudia Tanzania ikianguka kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA), Tanzania kwa sasa inashika nafasi ya 160 ikiwa ni nafasi mbaya kabisa kuwahi kushjka