Bokungu kuongezwa miezi sita Simba
Na Salum Fikiri Jr Dar es Salaam
Klabu ya Simba imesema itamuongezea mkataba wa mwingine wa miezi sita, beki wake wa kulia Janviel Besala Bokungu raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Bokungu atapewa mkataba huo mara baada ya kumalizika kwa huu mwingine wa miezi sita, Tayari Simba imeshamuongezea beki wake wa kushoto Mohamed Hussein 'Tshabalala' wa miaka miwili.
Bokungu aliyesajiliwa sambamba na Mkongo mwenzake Musa Ndusha, ameonyesha kiwango kikubwa katoka michezo kadhaa ambayo klabu yake ya Simba imecheza, endapo atapewa miezi sita, atalazimika kucheza hadi mwakani