Dula Mbabe kumbe dereva bodaboda!
Na Prince Hoza, Dar es Salaam
Mwanamasumbwi anayekuja juu kwa sasa hapa nchini Abdallah Pazi maarufu Dula Mbabe amefichua siri kwamba kabla hajajikita kwenye ndondi alikuwa dereva bodaboda.
Akizungumza katika kipindi cha michezo cha Sportaiment kinachorushwa na Sibuka FM, amesema aliingia kwenye ndondi kwakuwa alikuwa na kipaji cha kupigana tangu zamani.
Ila mchezo huo umempa nafasi kubwa ikiwemo kufahamika ndani na nje ya nchi, lakini kazi yake inayomuingizia kipato ni kuendesha bodaboda, bondia huyo hivi karibuni alimdunda Mchina kwa TKO