Bosi Azam afariki dunia
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Azam FC 'Wanalambalamba' Said Mohamed Abeid amefariki dunia katika hospitali ya Aga Khan iliyopo Dar es Salaam.
Mohamed ambaye ni makamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi na alilazwa katika hospitali hiyo.
Taratibu za mazishi zinafanywa na familia pamoja na Klabu yake na huenda akazikwa kesho, Mungu ailaze roho yake peponi, Amina