Leo ndio leo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika
Na Prince Hoza, Lubumbashi
Leo nyasi za uwanja wa Stade TP Mazembe mjini Lubumbashi hapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo zitawaka moto kwa miamba TP Mazembe watakapoialika Mo Bejaia ya Algeria katika mchezo wa fainali.
Timu hizo zilikutana Oktoba 29 mwaka huu katika dimba la Stade Mustapha Tchaker kule mjini Bejaia Algeria ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.
Kwa maana hiyo mchezo wa leo utakaopigwa saa 9:30 jioni TP Mazembe watahitaji sare isiyo na mabao ili waweze kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho, msimu uliopita Mazembe ilitwaa ubingwa wa Ligi ya mabingwa ambapo msimu huu waliondoshwa mapema