Wakala wa Jesse Were awaita mezani Yanga
Na Saida Salum, Dar es Salaam
Wakala wa mshambuliaji wa timu ya Zesco United ya Zambia Jesse Were raia wa Kenya, George Bwana amesema mchezaji wake yuko sokoni na anamuuza kwa kiasi kisichopungua Dola 150,000 sawa na shilingi Milioni 320 za Kitanzania.
Bwana amewaambia Yanga kuweka mezani kitita hicho ili straika huyo atue Jangwani, Were ni chaguo la kocha mpya wa Yanga, Mzambia George Lwandamina.
Tayari Yanga imeshamshusha kiungo mkata umeme wa Zesco United ya Zambia, Justin Zullu ambaye muda wowote atamwaga wino kuitumikia Klabu hiyo