Okwi aota mbawa Msimbazi
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Dili ya kumrejesha tena kwa mara ya pili mshambuliaji Emmanuel Okwi raia wa Uganda imekufa rasmi ama kwa lugha nyingine unaweza kusema imeota mbawa.
Okwi anayecheza soka la kulipwa nchini Denmark katika Klabu ya Sonderjsky inayoshiriki Ligi Kuu na michuano ya Ulaya, kiungo huyo mshambuliaji ilikuwa atue Simba kufuatia makubaliano mazuri waliyofikiana.
Lakini uongozi wa timu hiyo ukagoma kumwachia Okwi na sasa ataendelea kukipiga timu hiyo licha kwamba amekuwa akianzia benchi, taarifa za uhakika zinasema, Sondwrjsky walikuwa wakitaka walipwe kwanza Dola Laki mbili, na Simba ilikubali kufanya hivyo.
Ila mkurugenzi wa timu hiyo amesema timu yoyote inayomuhitaji Okwi lazima imnunue kwa fedha wanazohitaji wao ambazo ni zaidi ya Dola laki mbili, kwa maana hiyo Simba imeshindwa kumrejesha tena Okwi na sasa wanaangaza Zambia ambapo wamevamia katika timu ya Zesco United wakitaka kumchukua mshambuliaji wao John Chigandu