Simba sasa kuibomoa Zesco United, yamnasa mpachika mabao wao
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam
Baada ya kugonga mwamba kwa mshambulizi wake wa zamani Emmanuel Okwi, Simba imemgeukia mpachika mabao wa Zesco United ya Zambia, John Chingandu.
Taarifa zenye uhakika kutoka ndani ya Klabu hiyo zinasema Chingandu ni chaguo la kocha wao Mkameruni, Joseph Omog kwa maana hiyo nyota huyo anaweza kutua Msimbazi kuimarisha safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa haifanyi vizuri.
Haji Manara msemaji wa Klabu hiyo alikataa kuzungumzia hilo na kudai Simba inafanya usajili wake kimyakimya na wala mitandao ya kijamii haitaambiwa lolote, lakini Blogu hii imegundua janja ya timu hiyo kumnasa Chingandu ambaye ni mpachika mabao wa timu hiyo