Tusker mabingwa wapya Kenya

Na Mwandishi Wetu, Kenya

Ligi Kuu ya Kenya (KPL) nayo iliendelea katika viwanja tofauti mwishoni mwa juma lililopita katika uwanja wa Mumias Complex KK Homeboyz ilishindwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani pale ilipolazimishwa sare tasa 0-0 na Ulinzi Stars.

Lakini Sony Sugar ilikubali kichapo nyumbani cha mabao 2-1 na Posta Rangers, Mathare United ikitumia uwanja wa Nyayo Stadium ililazimishwa sare ya 2-2 na Sofapaka, wakati Thika United ikicheza kwenye uwanja wake wa Thika Stadium ilishinda 1-0 dhidi ya Chemell Sugar.

Kule mjini Mombasa, Bandari ikicheza kwenye uwanja wake wa Mbaraki Stadium ilishinda 1-0 dhidi ya Western Stima, Tusker FC nao wakatawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kenya baada ya kuilaza AFC Leopards bao 1-0, wakati Gor Mahia wakiwa ugenini waliibutua Muhoroni Youth kwa mabao 2-0 mechi ikipigwa Moi Stadium

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA