Orlando Pirates wamfuata Pluijm Yanga
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini imeweka bayana kwamba wanamchukua kocha anayetajwa kutemwa na mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Mholanzi Hans Van der Pluijm.
Maofisa wa Pirates wamekiri kumuhitaji Pluijm kwakuwa ni mmoja kati ua makocha bora wanaofaa kuinoa Klabu hiyo kubwa barani Afrika.
Licha kwamba Pluijm bado ni kocha wa Yanga, lakini ujio wa George Lwandamina wa Zesco United unapelekea Mdachi huyo kutimka Yanga kwakuwa amekataa kazi ya Ukurugenzi wa ufundi