Yanga yamsogelea mnyama kileleni

Na Ikram Khamees, Dar es Salaam

Yanga SC imeifunga Ruvu Shooting mabao 2-1 katika uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Ruvu Shooting walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Abdulraman Juma dakika ya saba kipindi cha kwanza, Lakini Yanga wakachomoa kwa bao la Simon Msuva.

Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa sare, kipindi cha pili Yanga wakaongeza bao la pili likifungwa na Haruna Niyonzima ambaye aling' ara, Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi 33 ikiwa nyuma ya pointi mbili na vinara Simba wenye pointi 35 huku zote zikicheza mechi 15, mzunguko wa kwanza ukimalizika rasmi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA