Mamelodi Sundowns washikwa, Orlando yaua

Na Mwandishi Wetu, Afrika Kusini

Mechi za mwishoni mwa wiki iliyopita hapa Afrika Kusini, Michuano ya Telkom Knockout iliendelea kwa mechi nne kupigwa karika viwanja tofauti.

Pale katika dimba la Orlando Stadium, wenyeji Orlando Pirates waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyowekwa kimiani na mshambuliaji wake hatari Ndoro, dhidi ya Highlanders Park ambao mfungaji wao ni Mvala aliyefunga dakika ya 66.

Mechi nyingine ilipigwa pale Lucas Moripe Stadium mabingwa wa Afrika, Mamelodi Subdowns wakishikwa shati na Supersport United baada ya kutoka sare tasa ya 0-0.

Lakini mechi ya kusisimua ilifanyika Peter Mokaba Stadium, Cape Town City Stars ikishinda mabao 4-3 dhidi ya wenyeji wao Baroka FC, Cape Town walianza kuandika magoli kupitia Majoro dakika ya 7, Jayiya dakika 20 na Mashikinya dakika ya 90, Baroka FC wakapata magoli yao matatu kupitia Mothuna dakika ya 45, Motshegwa dakika ya 59 na Mahashe dakika ya 90.

Cape Town City walipata bao la ushindi likifungwa na Masina dakika ya 114. Mechi nyingine ilipigwa Jumapili katika dimba la Moses Mabhida Stadium kati ya wenyeji Kaizer Chief na Free State Stars, mchezo huo uliisha kwa sare ya mabao 2-2 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA