Wimbo wa Kilevi changu, wampa dili Mkola Man
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Muda wowote msanii wa muziki wa kizazi kipya anayeishi Hale mkoani Tanga, Christopher Mhenga ama Mkola Man anaweza kuwa milionea kufuatia wimbo wake wa 'Kilevi changu' unaohamasisha matumizi ya sigara kununuliwa na kampuni ya Sigara (TCC).
Dili hilo limetokana na wimbo huo kusikika katika vituo kadhaa vya redio hivi karibuni na kuwavutia maofisa wa kampuni hiyo kubwa hapa nchini.
Msanii huyo aliyetoa nyimbo mbalimbali ambazo nyingine bado hazijasikika popote huenda akanufaika kwani inasemekana TCC inataka kuununua wimbo huo ili iweze kuuingiza kwenye matangazo yake