Simba ya mwendokasi kufumuliwa

Na Ikram Khamees, Dar es Salaam

Wekundu wa Msimbazi Simba SC maarufu kama 'mwendokasi' huenda wakakikosa kikosi chao hicho kufuatia fununu kwamba uongozi unataka kukifumua na kusajili wachezaji wengine huku taarifa zikienea kwamba Emmanuel Okwi anarejea.

Licha ya Okwi, inasemekana beki wa Azam FC, Shomary Kapombe naye anatajwa kurejea Msimbazi, Kapombe aliwahi kuichezea Simba misimu kadhaa iliyopita.

Mbali na wachezaji hao wa zamani, wakongwe wanaotajwa kurejea Simba ni Juma Kaseja na Haruna Moshi 'Boban' ambaye hata hivyo hakuna uhakika wa kusajiliwa tena, kipa wa JKT Ruvu Said Kipao anapewa nafasi ya kusajiliwa katika Dirisha dogo.

Aidha timu hiyo ambayo ndiyo vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ina npango wa kuwatema nyota wake watatu wa kigeni ambao ni Laudit Mavugo, Janviel Bokungu na Musa Ndusha

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA