Chuji Busungu, Seme nao kimeeleweka
Kiungo wa zamani wa Yanga na Simba Athuman Idd 'Chuji' amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na timu ya Ligi Kuu ya Ndanda FC ya mjini Mtwara. Chuji aliwahi kutamba kwenye vilabu vya Simba na Yanga kwa nyakati tofauti zote akizichezea mara mbili mbili, lakini alijiunga na Mwadui ya Shinyanga ambayo nayo aliachana nayo kabla ya msimu uliopita kujiunga na timu ya daraja la kwanza ya KCM ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Naye mshambuliaji wa zamani wa Mgambo JKT na Yanga, Malimi Busungu amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Lipuli ya mjini Iringa ambayo nayo itashiriki Ligi Kuu Bara. Wakati Busungu akisaini kujiunga na Lipuli, kiungo mwingine wa zamani wa Yanga na Ndanda, Omega Seme amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Lipuli Omega Seme, mwenye jezi nyekundu, akitambulishwa kujiunga na Lipuli Malimi Busungu (Katikati) akitambulishwa kutua Lipuli Athuman Idd "Chuji" akisaini Ndanda