Kabwili asaini Yanga miaka mitano

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Kipa chipukizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Ramadhan Kabwili amesaini mkataba wa miaka mitano kwa ajili ya kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC.

Kabwili atadumu na Yanga hadi mwaka 2022, kipa huyo chipukizi aliitwa kwenye timu ya taifa, Taifa Stars inayonolewa na Salum Mayanga kwa ajili ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani maarufu Chan.

Kabwili aliibukia kwenye timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu Serengeti Boys ambayo ilishiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo zilizofanyika mapema mwaka huu nchini Gabon, kipa huyo aliweza kushiriki mechi zote katika kikosi cha kwanza na ndipo Yanga ilipomuona na kuamua kumnasa

Kipa wa Serengeti Boys, Ramadhan Kabwili amesaini Yanga miaka mitano

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA