Kilichomvua unahodha Mkude hiki hapa

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Siku moja baada ya kuvuliwa unahodha wa Simba Jonas Mkude na kukabidhiwa Mzimbabwe Method Mwanjale atakayesaidiana na John Bocco "Adebayor" na Mohamed Hussein "Tshabalala", siri imefichuka.

Taarifa ambazo zina uhakika kabisa kutoka Msimbazi zinasema kuwa Mkude amevuliwa unahodha baada ya kuhangaishana na mabosi wa timu hiyo katika suala la kuongeza mkataba.

Inasemekana mchezaji huyo alikuwa rafiki mkubwa wa mshambuliaji Ibrahim Ajibu aliyejiunga na Yanga na wote lao lilikuwa moja ambapo kila mmoja alitaka dau kubwa zaidi ili wasalie Msimbazi na Ajibu aliamua ajiunge na Yanga baada ya Simba kukataa kumpa dau hilo.

Ilikuwa chupuchupu Mkude naye aende Yanga kama ilivyo kwa Ajibu, hapo ndipo alipoanza kuwachefua mabosi wa Simba na walipokamilisha kandarasi wakaamua kumpoka unahodha kwani siku zote nahodha huwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja

Jonas Mkude amevuliwa unahodha

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA