SIMBA YAMALIZANA NA MANULA, APAA

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam.

Hatimaye klabu ya Simba imekamilisha usajili wa mlinda mlango namba moja hapa nchini Aishi Salum Manula ambaye pia ni mchezaji wa Azam FC na timu ya taifa, Taifa Stars, Manula amesaini Simba mkataba wa miaka miwili.

Minong' ono ilikuwa mingi kwamba kipa huyo asingejiunga Simba lakini Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara akathibitisha kuwa kipa huyo sasa ni mali ya Simba na anakuwa mchezaji wa 13 kusajiliwa na kikosi hicho huku huenda Haruna Niyonzima naye akatambulishwa.

Manula atapaa kesho kuelekea Afrika Kusini ambako wenzake wapo huko wakijifua kwa kambi maalum ya kujiandaa na msimu mpya, Manula atakuwa na kazi ngumu kukaa langoni kwakuwa atakuwa sambamba na kipa mwenzake wa Stars, Said Mohamed Nduda

Aishi Manula amejiunga Simba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA