Simba kuanza kucheza na Orlando, Bidvest

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Timu ya soka ya Simba SC, ya jijini Dar es Salaam ambayo kwa sasa imeweka kambi yake nchini Afrika Kusini ikiwa katika maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Haji Manara amesema Wekundu hao wanatarajia kushuka viwanjani kucheza mechi za kujipima nguvu.

Simba itacheza na Orlando Pirates kisha itacheza na Bidvest Wits ambazo zote zinashiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, mechi hizo zitachezwa juma lijalo na Simba itamaliza ziara yake kisha itarejea Dar es Salaam kucheza mechi nyingine ya kirafiki kuadhimisha Simba Day

Wachezaji wa Simba wakijifua

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA