AVEVA, KABURU NAO KUSOTA HADI AGOSTI 7
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Mahakama ya Kisutu leo imeipiga tena kalenda kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa klabu ya Simba, Rais Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange Kaburu ambapo sasa wamerudishwa rumande hadi Agosti 7 mwaka huu wakati kesi yao itakaposikilizwa tena.
Wawili hao wanakabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha ambapo kisheria wanakosa dhamana, Aveva na Kaburu leo wote wamefika mahakamani tofauti na Julai 21 ambapo Kaburu hakufika mahakamani alikuwa akiugua ghafla.
Kusogezwa mbele kwa kesi hiyo kunapisha kukamilika kwa upepelezi na kama ukikamilika basi kuna uwezekano wawili hao wakahukumiwa na kama usipokamilika kuna uwezekano wa kuendelea kusota mahabusu